Genesis 31:45-50

45Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. 46Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. 47Labani akaliita Yegar-Sahadutha
Yegar-Sahadutha maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiaramu.
na Yakobo akaliita Galeedi.
Galeedi maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiebrania.

48Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. 49Pia liliitwa Mispa,
Mispa maana yake Mnara wa ulinzi.
kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.
50Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

Copyright information for SwhKC